Hatimaye mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia 2014 Brazil ametupwa nje ya michuano hiyo baada ya kuchezea kichapo kizito cha mabao 7-1 kutoka kwa ujerumani katika mechi ya nusu fainali ya kwanza.Ujerumani walianza sherehe ya magoli kupitia kwa mshambuliaji wake Thomas muller aliyefunga mawili,mabao mengine yalifungwa na miroslav klose(moja) tom kroos(moja) sami khedira(moja) schuerrle(mawili) na bao la kufutia machozi kwa upande wa Brazil liliwekwa kimiani na oscar.Baada ya kufunga goli moja katika mchezo huo mshambuliaji miroslav klose amevunja rekodi ya ronaldo de lima hvyo kwa sasa yeye ndio kinara wa mabao kwa vipindi vote vya michuano ya kombe la dunia.
No comments:
Post a Comment