Wednesday, July 9, 2014

FAINALI NI UJERUMANI NA ARGENTINA ,UHOLANZI YAONDOLEWA KWA MIKWAJU YA PENATI

Argentina imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya kombe la dunia baada ya kuin'goa uholanzi kwa mikwaju ya penati kufuatia matokeo ya bila kufungana ndani ya dakika 120,pongezi kwa golikipa wa  Argentina sergio romero kwa kupangua penati mbili ya wesley sneijder na ron vlaar wachezaji arjen robben na dirk kuyt walipata penati hizo na kwa upande wa Argentina penati zao ziliwekwa kimiani na maxi Rodriguez,Lionel messi,ezequiel galay na Sergio aguero na kufanya matokeo kuwa 4-2 kwa hiyo Argentina itacheza fainali na ujerumani wakati uholanzi itacheza dhidi ya brazil kuwania nafasi ya mshindi wa tatu.

No comments:

Post a Comment