Michuano ya kombe la dunia inatarajiwa kuendelea leo nchini Brazil ambapo mwenyeji wa michuano hiyo Brazil atakipiga dhidi ya uholanzi katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu kocha wa Brazil Luis Felipe Scolari amesema ni wakati sasa wa kurejesha heshima ya nchi baada ya kupata kipigo cha aibu cha mabao 7-1 kutoka kwa ujerumani katika mchezo wa nusu fainali naye nahodha wa timu hiyo thiago silva leo atarejea dimbani baada ya kukosekana kwenye mchezo dhidi ya ujerumani kwa kua alikuwa na kadi mbili za njano, thiago amesema ni muda wa mashabiki wa Brazil kusahau yaliyopita na kuwaunga mkono wachezaji wa timu hiyo ambao wameahidi watacheza kama fainali ili waweze kupata ushindi.
No comments:
Post a Comment