Monday, August 11, 2014

KLOSE ATUNDIKA DARUGA SOKA LA KIMATAIFA

Mchezaji anayeshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi kwa nyakati zote za kombe la dunia mjerumani Miroslav Klose amestaafu kuichezea timu ya taifa ya ujerumani,katika kombe la dunia lililomalizika hivi karibuni klose alifunga mabao mawili na kufikisha idadi ya mabao 16 na kuvunja rekodi ya ronaldo de lima hvyo amekua kinara wa ufungaji katika vipindi vyote vya kombe la dunia "nna furaha kufikia mafanikio haya hakika nimeacha nyakati nyingi za kukumbukwa" alisema klose mwenye miaka 36 mpaka anastaafu klose ameifungia ujerumani  mabao 71.

Friday, July 18, 2014

PHILIP LAHM ATUNDIKA DARUGA SOKA LA KIMATAIFA

Nahodha aliyeiongoza ujerumani kutwaa kombe la dunia nchini brazil Philip Lahm amestaafu kuichezea timu ya taifa ya ujerumani mchezaji huyo mwenye miaka 30 alimpa taarifa kocha wa ujerumani Joachim low na pia alituma barua kwa chama cha soka cha ujerumani, Lahm alianza kua nahodha wa kikosi cha ujerumani mwaka 2010 baada ya aliyekua nahodha wa timu hiyo Michael Ballack kuumia  kwenye kombe la dunia lililofanyika nchini africa kusini,mshambuliaji wa arsenal Lukas podolski baada ya kupata taarifa ya kustaafu kwa lahm alisema "ilikua ni furaha sana kucheza timu moja na wewe".

CHELSEA YANASA KIFAA KINGINE KUTOKA ATLETICO MADRID

Beki wa kushoto wa atletico Madrid Felipe Luis raia wa brazil amesajiliwa na chelsea kwa dau la euro milioni 15 baada ya kukamisha usajili huo Luis alisema "ndoto yangu imetimia sasa naweza kuichezea Chelsea na pia ligi kuu ya uingereza na nitacheza kwa bidii ili kuisaidia timu kufanya vizuri" Luis mwenye miaka 28 anakua mchezaji wa pili kusajiliwa na Chelsea kutoka atletico madrid baada ya kumsajili Diego Costa miezi michache iliyopita

FERDINAND ASAINI QPR

beki  aliyetemwa na manchester united  Rio Ferdinand amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea timu ya Queens park rangers ambayo imepanda daraja Ferdinand mwenye miaka 35 alifanya mazungumzo na kocha wa timu hiyo Harry Redknapp kwenye moja ya hoteli kubwa jijini London,Rio atalipwa mshahara wa pauni 70000.

Thursday, July 17, 2014

ARSENAL YAMNASA DEBUCHY

Klabu ya arsenal imefanikiwa kunasa saini ya beki wa kulia wa Newcastle united Mathieu debuchy raia wa ufaransa kwa kitita cha paundi milioni 12 debuchy amesajiliwa na arsenal ili kuziba pengo la beki wa kulia lililoachwa na mfaransa mwenzie bacary sagna aliyetimkia manchester city debuchy amesema "nimefurahi kujiunga na arsenal sababu ni moja kati ya timu kubwa duniani na ninaahidi kuisaida kunyakua mataji mbalimbali" naye kocha wa arsenal arsene wenger amesema ana imani uzoefu wa debuchy utaisaidia arsenal kufanya vizuri msimu ujao.

REAL MADRID YAMNASA TONI KROOS

Klabu ya real madrid ya hispania imefanikiwa kunasa saini ya kiungo wa Bayern Munich Toni kroos kwa ada ya uhamisho pauni milioni 24 mchezaji huyo mwenye mwenye miaka 24 raia wa ujerumani amesaini mkataba wa miaka sita kuichezea timu hiyo naye mwenyekiti wa bayern munich Karl-heinz Rummenigge amesema "tunamshukuru kroos kwa mchango wake tunamtakia maisha mema yeye na familia yake wakiwa real madrid".

MWOMBEKI WA SIMBA ATUA JKT RUVU

Mchezaji betram mwombeki aliyechezea simba mechi chache za mzunguko wa pili msimu uliopita leo alionekana viwanja vya azam complex akiwa amevalia uzi wa JKT RUVU wakati timu hiyo ilipocheza na Azam FC kocha Fred Felix Minziro alimpanga katika mechi hiyo iliyoisha kwa matokeo ya azam kushinda magoli 2-1 na mwombeki ndiye aliyetoa pasi ya goli la JKT RUVU..mwombeki alipoulizwa alisema "ndio niko hapa naangalia ustaarabu mpya" nae meneja wa timu hiyo alisema tumempokea mwombeki na tunafanya nae mazungumzo ili tuweze kumsajili. :picha kwa hisani ya bin zubery

AZAM YAIBAMIZA JKT RUVU 2-1

Timu ya soka ya Azam FC leo imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya JKT RUVU kwenye uwanja wa azam complex na kufanikiwa kushinda mabao 2-1 mabao hayo yaliwekwa kimiani na kipre tchetche(nahodha) pamoja na mshambuliaji aliyesajiliwa kutoka yanga didier kavumbagu huku bao la kufutia machozi kwa upande wa JKT RUVU likifungwa na Hassan Bilal, hiyo ni mechi ya kirafiki ya tatu mfululizo kwa azam kuibuka na ushindi baada ya kuifunga kombaini ya jeshi 3-0 kabla ya kuichapa polisi morogoro 1-0:picha kwa hisani ya bin zubeiry.

Wednesday, July 16, 2014

VAN GAAL ATAMBULISHWA RASMI MAN UNITED

kocha mpya wa Manchester united Luis van gaal ametambulishwa rasmi na klabu hiyo hapo Jana kwenye uwanja wa mazoezi wa timu hiyo carrigton park,kocha huyo alitambulishwa na makamu mwenyekiti wa timu hiyo Ed Woodward na kocha msaidizi wa timu hiyo Ryan Giggs.

JAJA AANZA KUJIFUA YANGA

mshambuliaji aliyesajiliwa na yanga kutoka nchini Brazil Geilson Santana Santos ameanza kujifua na wenzake leo asubuhi  kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya loyola :picha kwa hisani ya binzubery.

Tuesday, July 15, 2014

LIVERPOOL YAMSAJILI MARKOVIC WA BENFICA

Klabu ya soka ya Liverpool ya nchini england imemsajili mchezaji raia wa serbia   Lazar marckovic kwa dau la pauni milioni 20 mchezaji huyo aliyetokea benfica ya ureno aliisaidia timu hiyo kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya nchi hiyo msimu uliopita na kwa sasa anakamilisha idadi ya wachezaji wanne waliosajiliwa na Liverpool kwa ajili ya msimu ujao wengine wakiwa ni Adam lallana,Rickie Lambert wakitokea southampton pamoja na Emre can aliyetokea Bayer leverkusen, "nimefurahi kujiunga na klabu kubwa kama hii" alisema marckovic baada ya kukamilisha usajili wake.

MBRAZIL MWINGINE ATUA YANGA

Timu ya soka ya dar-es-salaam young africans imemsajili mshambuliaji Geilson Santos Santana "jaja" kutoka Brazil,jaja mwenye miaka 28 aliyekua akiichezea klabu ya itabaina FC ya brazil anakua mchezaji wa pili kutoka nchini brazil kusajiliwa na yanga mchezaji huyo amewasili leo mchana akitokea sao paulo nchini brazil hivyo ataungana na  wabrazil wenzie makocha Marcio maximo na  Leonardo neiva pamoja na mchezaji Andrey coutinho,yanga wamefanya usajili huo ili kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya michuano ya kombe la kagame itakayofanyika Kigali nchini Rwanda,ligi kuu ya vodacom Tanzania bara pamoja na michuano ya kombe la shirikisho barani africa.

Monday, July 14, 2014

WACHEZAJI WA UJERUMANI WAPONGEZWA KWA MABUSU MOTO MOTO NA WAPENZI WAO

Baada ya kutwaa kombe la dunia kwa kuifunga Argentina bao 1-0 baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya ujerumani walipongezwa kwa mabusu motomoto na wapenzi wao miongoni mwa wachezaji hao ni sami khedira,mats hummels,schuerrle ambae alionekana kuona aibu kwenye suala hilo.,pamoja na muuaji Mario gotze.

SCOLARI ATUPIWA VIRAGO

kocha aliyekua akiinoa timu ya taifa ya brazil luis Felipe scolari ametimuliwa baada ya Brazil kufanya vibaya katika michuano ya kombe la dunia inadaiwa kocha huyo alikutana na uongozi wa chama cha soka cha brazil CBF jumamosi usiku baada ya kupata kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa uholanzi na kupewa barua ya kutimuliwa.

FRED WA BRAZIL ASTAAFU KUICHEZEA TIMU YA TAIFA

Baada kuonyesha kiwango kibovu kwenye kombe la dunia mshambuliaji wa timu ya taifa ya brazil mwenye miaka 30 FRED amestaafu kuichezea timu hiyo baada ya mashabiki wa timu hiyo kutoridhishwa na kiwango chake jambo lililopelekea kuzomewa mara kwa mara kwenye michuano ya kombe la dunia hususani kwenye  mechi ya Brazil dhidi ya ujerumani ambapo Brazil ilifungwa mabao 7-1 mpaka anaastaafu FRED ameichezea timu hiyo mechi 39.

Sunday, July 13, 2014

UJERUMANI YATWAA KOMBE LA DUNIA

Timu ya taifa ya ujerumani imetwaa ubingwa wa kombe la dunia baada ya kuifunga Argentina bao  1-0 bao lililofungwa na mshambuliaji wa klabu ya Bayern munich Mario Gotze aliyeingia dakika ya 88 kuchukua nafasi ya miroslav klose  ujerumani ilibidi wasubiri hadi dakika ya 112 na kuweza kujipatia bao hilo baada ya kutoka sare ya bila kufungana

Saturday, July 12, 2014

KOMBE LA DUNIA NI BRAZIL DHIDI YA UHOLANZI LEO

Michuano ya kombe la dunia inatarajiwa kuendelea leo nchini Brazil ambapo mwenyeji wa michuano hiyo Brazil atakipiga dhidi ya uholanzi katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu kocha wa Brazil Luis Felipe Scolari amesema ni wakati sasa wa kurejesha heshima ya nchi baada ya kupata kipigo cha aibu cha mabao 7-1 kutoka kwa ujerumani katika mchezo wa nusu fainali naye nahodha wa timu hiyo thiago silva leo atarejea dimbani baada ya kukosekana kwenye mchezo dhidi ya ujerumani kwa kua alikuwa na kadi mbili za njano, thiago amesema ni muda wa mashabiki wa  Brazil kusahau yaliyopita na kuwaunga mkono wachezaji wa timu hiyo ambao wameahidi watacheza kama fainali ili waweze kupata ushindi.

Friday, July 11, 2014

BREAKING NEWS:SUAREZ ASAINI RASMI BARCELONA

klabu ya Barcelona imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji wa liverpool Luis Suarez kwa ada ya uhamisho paundi milioni 75 na imemkabidhi jezi namba 9 Suarez amewaomba radhi mashabiki wa Liverpool kwani ilikua ni ndoto yake ya muda mrefu kucheza soka nchini hispania lakini pia atakua karibu na familia yake pamoja na mke wake sophia mwisho aliwatakia kila la heri liverpool naye kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amemshukuru Suarez kwa mchango wake ulioifanya timu kurudi kwenye michuano ya klabu bingwa barani ulaya(uefa champions league) lakini Suarez hatatambulishwa na Barcelona kutokana na adhabu anayoitumikia ya kutojihusisha na masuala ya soka kwa muda wa miezi minne kwa kosa la kumn'gata Giorgio chiellini kwenye mechi ya kombe la dunia

FIFA YAKATAA RUFAA YA SUAREZ

FIFA imeipiga chini rufaa ya chama cha soka cha uruguay AUF iliyomkatia mchezaji wake Luis suarez baada ya kumn'gata beki wa italia giorgio chiellini kwenye mechi ya kombe la dunia pia FIFA imeambatanisha adhabu hiyo na faini ya paundi 100,000