Mchezaji anayeshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi kwa nyakati zote za kombe la dunia mjerumani Miroslav Klose amestaafu kuichezea timu ya taifa ya ujerumani,katika kombe la dunia lililomalizika hivi karibuni klose alifunga mabao mawili na kufikisha idadi ya mabao 16 na kuvunja rekodi ya ronaldo de lima hvyo amekua kinara wa ufungaji katika vipindi vyote vya kombe la dunia "nna furaha kufikia mafanikio haya hakika nimeacha nyakati nyingi za kukumbukwa" alisema klose mwenye miaka 36 mpaka anastaafu klose ameifungia ujerumani mabao 71.
erick updates
Monday, August 11, 2014
Friday, July 18, 2014
PHILIP LAHM ATUNDIKA DARUGA SOKA LA KIMATAIFA
Nahodha aliyeiongoza ujerumani kutwaa kombe la dunia nchini brazil Philip Lahm amestaafu kuichezea timu ya taifa ya ujerumani mchezaji huyo mwenye miaka 30 alimpa taarifa kocha wa ujerumani Joachim low na pia alituma barua kwa chama cha soka cha ujerumani, Lahm alianza kua nahodha wa kikosi cha ujerumani mwaka 2010 baada ya aliyekua nahodha wa timu hiyo Michael Ballack kuumia kwenye kombe la dunia lililofanyika nchini africa kusini,mshambuliaji wa arsenal Lukas podolski baada ya kupata taarifa ya kustaafu kwa lahm alisema "ilikua ni furaha sana kucheza timu moja na wewe".
CHELSEA YANASA KIFAA KINGINE KUTOKA ATLETICO MADRID
Beki wa kushoto wa atletico Madrid Felipe Luis raia wa brazil amesajiliwa na chelsea kwa dau la euro milioni 15 baada ya kukamisha usajili huo Luis alisema "ndoto yangu imetimia sasa naweza kuichezea Chelsea na pia ligi kuu ya uingereza na nitacheza kwa bidii ili kuisaidia timu kufanya vizuri" Luis mwenye miaka 28 anakua mchezaji wa pili kusajiliwa na Chelsea kutoka atletico madrid baada ya kumsajili Diego Costa miezi michache iliyopita
FERDINAND ASAINI QPR
beki aliyetemwa na manchester united Rio Ferdinand amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea timu ya Queens park rangers ambayo imepanda daraja Ferdinand mwenye miaka 35 alifanya mazungumzo na kocha wa timu hiyo Harry Redknapp kwenye moja ya hoteli kubwa jijini London,Rio atalipwa mshahara wa pauni 70000.
Thursday, July 17, 2014
ARSENAL YAMNASA DEBUCHY
Klabu ya arsenal imefanikiwa kunasa saini ya beki wa kulia wa Newcastle united Mathieu debuchy raia wa ufaransa kwa kitita cha paundi milioni 12 debuchy amesajiliwa na arsenal ili kuziba pengo la beki wa kulia lililoachwa na mfaransa mwenzie bacary sagna aliyetimkia manchester city debuchy amesema "nimefurahi kujiunga na arsenal sababu ni moja kati ya timu kubwa duniani na ninaahidi kuisaida kunyakua mataji mbalimbali" naye kocha wa arsenal arsene wenger amesema ana imani uzoefu wa debuchy utaisaidia arsenal kufanya vizuri msimu ujao.
REAL MADRID YAMNASA TONI KROOS
Klabu ya real madrid ya hispania imefanikiwa kunasa saini ya kiungo wa Bayern Munich Toni kroos kwa ada ya uhamisho pauni milioni 24 mchezaji huyo mwenye mwenye miaka 24 raia wa ujerumani amesaini mkataba wa miaka sita kuichezea timu hiyo naye mwenyekiti wa bayern munich Karl-heinz Rummenigge amesema "tunamshukuru kroos kwa mchango wake tunamtakia maisha mema yeye na familia yake wakiwa real madrid".
MWOMBEKI WA SIMBA ATUA JKT RUVU
Mchezaji betram mwombeki aliyechezea simba mechi chache za mzunguko wa pili msimu uliopita leo alionekana viwanja vya azam complex akiwa amevalia uzi wa JKT RUVU wakati timu hiyo ilipocheza na Azam FC kocha Fred Felix Minziro alimpanga katika mechi hiyo iliyoisha kwa matokeo ya azam kushinda magoli 2-1 na mwombeki ndiye aliyetoa pasi ya goli la JKT RUVU..mwombeki alipoulizwa alisema "ndio niko hapa naangalia ustaarabu mpya" nae meneja wa timu hiyo alisema tumempokea mwombeki na tunafanya nae mazungumzo ili tuweze kumsajili. :picha kwa hisani ya bin zubery